HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 1, 2017

NAHREEL NA WASANII WENGINE WA MUZIKI WAENDELEA KUSUKA KOLABO COKE STUDIO 2017

 Msanii wa Bongo Fleva, Nahreel aniwa na Aika (wa kwanza kulia) akiwa na wasanii wenzake katika studio za Coke Studio jijini Nairobi nchini Kenya.
Msanii Nahreel.

Mtayarishaji wa muziki na mwanamuziki nguli nchini Nahreel , akishirikiana na magwiji wengine wa kutengeneza muziki barani Afrika wanaendelea kusuka kolabo za wanamuziki wanaoshiriki onyesho la Coke studio linalotarajiwa kuanza kuonyeshwa kwenye vituo vya luninga mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Ms ambaye jina lake halisi ni, Emmanue Mkono, amefanya nyimbo nyingi bora za wasanii mbalimbali nchini ambazo zinatamba katika soko la muziki ndani na nje ya nchi pia ni mmoja wa wanamuziki wa kundi machachari la NEVY KENZO.

Akiongea kuhusu onyesho hili akiwa jijini Nairobi nchini Kenya, Nahreel amesema kuwa misimu minne ya Coke Studio Africa imekuwa na mafanikio makubwa katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava barani Afrika. Washiriki wamejiongezea mashabiki, wamejifunza mambo mengi kuhusu muziki kama burudani, muziki kama taaluma na muziki kama biashara na tena si tu kutoka kwa wasanii wenzao wa Afrika, bali wa Marekani pia.

Baadhi ya wakali wa kutengeneza muziki anaoshirikiana nao msimu huu ni Yuvir Pillay Nivedan a.k.a Sketchy Bongo kutoka Afrika ya Kusini na Kiff No beat kutoka nchini Ivory Coast.

Kwa upande wa ma DJ wapo Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius, Jah Prayzah na Slapdee from Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana, Betty G kutoka Ethiopia, Bruce Melodie, Shellsy Baronet na Mr. Bow kutoka Msumbiji , Denise kutoka Madagascar ,Ozane kutoka Togo na Freeda kutoka Namibia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Coca-Cola msimu wa Coke Studio mwaka huu utakuwa umesheheni burudani za muziki motomoto wenye vionjo vya Kiafrika kutokana na kuwaweka wasanii pamoja kutoka nchi 16 za Afrika na kushirikiana kufanya kolabo ambapo onyesho lake litaonyeshwa kwenye vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika.

Wasanii wanaoshiriki Coke Studio msimu huu wanatokea katika nchi za Africa ya Kusini, Rwanda, Angola, Zimbabwe, Togo, Madagascar, Mauritius, Kenya, Uganda, Tanzania, Nigeria, Ghana, Msumbiji, DRC, Ethiopia, Cameroon. The last edition featured Kenya, Uganda, Tanzania, Nigeria, Ghana, Mozambique, DRC, Ethiopia, Cameroon, Cote d’ Ivoire, and Togo.

Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

Wasanii wa Tanzania wanaoshiriki msimu huu wa Coke Studio 2017 ambao watafanya kolabo na wanamuziki kutoka nchini nyingine za Afrika ni Rayvanny, Izzo Bizness, Ali Kiba, na Nandy.Baadhi ya wasanii wakali wengine kutoka Tanzania waliowahi kushiriki onyesho hili ni Lady Jay Dee,Diamond Platinumz,Vanessa Mdee,John Makini,Shaa ,Ben Paul,Fid Q na kikundi cha Zanzibar Culture music Taarabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad