HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 August 2017

MWANZA: MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI KWIMBA.

KWAMBA TAREHE 21/08/2017 MAJIRA YA 08:45HRS ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA BUSULWA KATA YA NGULLA WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, LEONARD MATHIAS MIAKA 23, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUCHOMWA MOTO HADI KUPOTEZA MAISHA KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WATANO MALI YA ESTER ROBERT, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALIIBA KUKU WATANO NYUMBANI KWA BI ESTER ROBERT KIJIJINI NGULLA KISHA ALIKIMBILIA KIJIJI CHA JIRANI CHA MWABOMBA. INADAIWA KUWA  WANANCHI WA KIJIJI CHA MWABOMBA WALIPOMUONA MAREHEMU AKIWA NA KUKU HAO WALIPATA MASHAKA KISHA WALIMKAMATA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KIJIJI CHA NGULLA NDIPO MWENYE KUKU BI ESTER ROBERT ALIFIKA NA KUKABIDHIWA KUKU WAKE.

INADAIWA KUWA BAADA YA MAREHEMU KUKABIDHI KUKU KWA MWENYE MALI, WANANCHI WALIMCHUKUA NA KWENDA NAE KITUO CHA POLISI LAKINI WAKIWA NJIANI WALIANZA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BAADAE KUMCHOMA MOTO. POLISI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NDIPO WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO NA TUKIO NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU SABA AMBAO WANADAIWA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO WATUHUMIWA SABA WALIOKAMATWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA KISHA IKITHIBITIKA WATUHUMIWA WALIHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO BADO UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOMKAMATA WAHALIFU AU MHALIFU WAMPELEKE KWENYE KITUO CHA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. PIA ANAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad