Mtaa Kwa Mtaa Blog

MCT Yatangaza Ripoti ya Uchunguzi wa Uvamizi wa Studio za Clouds TV

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma.
Pia Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa uhariri.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya habari na kwamba hambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.

“Hatujafanya uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget