HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 17 August 2017

Mbunge CHADEMA ‘kuwalilia’ bodaboda bungeni

Mbunge wa viti maalumu (Chadema) mkoani Geita, Upendo Peneza amesema atapeleka maombi bungeni kuliomba bunge kupitia upya sheria za usalama barabarani ikiwamo faini kwa waendesha bodaboda ili ziweze kupunguzwa.
Peneza ameyasema hayo baada ya kupokea kilio cha waendesha bodaboda wa mji wa Geita waliolalamikia faini wanazotozwa ambazo hazilingani na chombo cha usafiri wanachotumia.
Waendesha bodaboda hao wamedai faini ya Sh30,000 kwa kosa moja ambayo inalinganishwa sawa na gari ni kubwa kwa kuwa kipato chao hakilingani na kipato cha anaeyeendesha gari.
Kutokana na ombi hilo, Peneza amesema atapeleka ombi bungeni kama mwakilishi wa wananchi kuomba sheria ambazo sio rafiki kwa bodaboda zirudishe bungeni kwa ajili ya marekebisho.
“Mimi malalamiko yote nimeyapokea nitafanyia kazi kama mwakilishi wao nitajitahidi kuhakikisha sheria zote ambazo sio rafiki nitaomba ziletewe bungeni ili zifanyiwe marekebisho lakini pia niwaombe kaka zangu hawa wa bodaboda wajitahidi kufanya kazi kwa kutii sheria wajue pia wajibu wao,” amesema Peneza.
Peneza ambaye alipita kwenye maeneo ya vijiwe vya bodaboda na kugawa “reflector” kwa zaidi ya waendesha bodaboda 400 wa mjini Geita, amesema lengo lake kubwa ni kuwasaidia vijana hao walioamua kujiajiri kufanya kazi kwenye mazingira rafiki na kuona ni namna gani ya kutatua kero zinazowakabili.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad