HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 24 August 2017

MASHINDANO YA GOFU AFRIKA MASHARIKI YAANZA KUTIMUA VUMBI LEO


MCHEZAJI wa Timu ya Gofu ya Tanzania, Amani Said, akipiga mpira katika Shimo Namba 9, wakati akichuana na mpinzani wake John Karichu, kutoka nchini Kenya, katika mashindano ya Tano ya Kanda ya Afrika Mashariki yanayoshirikisha Nchi Sita za Tanzania, Ethiopia, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, yaliyoanza jana katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

JUMLA ya nchi Sita leo zimeanza mchuano mkali katika mashindano ya gofu ya kanda ya tano ya Afrika yaliaonza kutimua vumbi katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya siku tatu yaliyoanza jana yanazishirikisha nchi za Rwanda,Burundi,Ethiopia,Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania.

Katika mchezo uliochezwa jana upande wa ‘Singel’s kati ya Amani saidi kutoka Tanzania na John Karicho kutoka Kenya wachezaji hao walitoka sare katika mashimo 18 waliyocheza.

Akizungumza  baada ya mchuano huo kumalizika, Karicho kutoka Kenya, alisema kuwa mchuano ulikuwa mzuri na wenye upinzani mkubwa kutokana jinsi alivyokuwa nyuma kwa viwanja 3-0 kati ya viwanja 9 walivyocheza.
Aidha Karicho, alisema kuwa uchezaji wa mpinzani wake, Saidi ni mzuri sana na katika mchezo huo alidai alicheza kwa uangalifu mkubwa katika viwanja 9 vya mwisho kuhakikisha anasawazisha matokeo hayo.Kwa upande wake Said, alisema kuwa angeweza kurudi na ushindi kama angecheza vizuri katika viwanja 9 vya mwisho. “Nimeshangaa sana kwa matokeo haya na sikutegemea kabisa kama mpinzani wangu angeweza kutoa sare na mimi kwa jinsi nilivyokuwa nimembana,”alisema Saidi.


Hata hivyo licha ya Amani Saidi kutoka sare katika mchezo wake naye Nahodha wa Tanzania Victor Joseph aliweza kumshinda kirahisi Baguma Richard kutoka Uganda kwa viwanja 8-7.

 Joseph alisema kuwa, hakupata upinzani katika mchezo wake katika viwanja hivyo walivyocheza.
“Niliingia uwanjani kwa kutomdharau mpinzani wangu nilicheza kwa madhumuni ya kuhakikisha namshinda mapema mpinzani wangu,”alisema Joseph.


Hata hivyo Joseph alisema kuwa anayaona mashindano hayo ya mwaka huu kama yatakuwa magumu zaidi kulinganisha na mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika Ethiopia.


Katika mchezo mwingine Abdul Dyabar, kutoka Uganda alimshinda Glslassie Ephrem, kutoka Ethiopia kwa 7-0.

Watanzania wengine waliotarajia kucheza jana jioni ni Seif Mcharo na N. Emanuel kutoka Rwanda,Prosper Herman na Salumu Hakizimana wa Burundi,Richard Mteve na Abdul Bizimana Burundi, ambapo mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Pravir Singh Ghattora na Krova Nahimana wa Burundi.
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofika kushuhudia mchuano huo


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad