HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 19 August 2017

EFM YATINGA RASMI MBEYA, YATOWA MAFUTA KWA VYOMBO VYA USAFIRI VYENYE STIKA YA 103.3 EFM.

 Meneja mkuu wa Redio ya E.fm Ndugu, Denis Busulwa akiwapa vipande wapinzani wake katika mtanange kati ya timu ya E.Fm Redio na timu ya Viongozi wa Serikali katika mchezo ulio chezwa hii leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini mbeya ambapo Timu Ya EFm iliongoza kwa kuibugiza Timu ya Viongozi wa Serikali Gori 6-1.
Efm redio 103.3 fm imekuja Mbeya rasmi, ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto venye stika ya 103.3 Efm Mbeya. ambapo kila pikipiki, bajaji na magari iliwekewa mafuta full tank. ikiwa na Shamra shamra za kituo hicho cha redio kuingia rasmi kusikika kwa kishindo mkoani mbeya kupitia mawimbi ya 103.3 fM.
 Kutoka kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Mohamed Mpinga akizungumza jambo kwa wachezaji wa Timu ya Efm Redio Pamoja na Timu ya Viongozi wa serikali hawapo pichani kabla ya mchezo kuanza.

Kutoka kushoto ni  Meneja mkuu wa Redio ya E.fm Ndugu, Denis Busulwa akipokea zawadi ya Tsheti kutoka kwa wadau na wasikilizaji wa 103.3 Efm Redio Mbeya
Vile vile siku ya Leo kulikua na jogging club asubuhi na wakazi wa Mbeya kwa lengo la kuhamasisha mazoezi kwa wakazi wa mbeya ili kujijenga kimwili na kiafya kama ambavyo Efm Redio ikifanya mazoezi hayo kila siku jijini Dar es salaam.
madereva wa pikipiki wakisubiri zawadi ya mafuta kutoka Efm redio 103.3 fm , ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto venye stika ya 103.3 Efm Mbeya. ambapo kila pikipiki na bajaj iliopata fursa hiyo iliwekewa mafuta full tank. 
PICHA NA MR.PENGO - MBEYA.
Mechi ya utangulizi Kati ya Wadau na Mashabi kinazi wa Timu ya Mbeya City wakoma kumwanyaa na Mashabiki kinazi wa Timu ya wajelajela Tanzania Prison walichuwana vikali kabya ya mtanange wa Timu ya Efm Redio Na Timu Ya Viongozi wa Serikali Kuanza.
Hivi ndivyo mambo yalivyo noga kwa mwendo wa Kwi...kwi kutoka  103.3 Efm Redio Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad