HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 18 August 2017

BENKI YA FINCA KUBORESHA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WATEJA WAKE.

Benki ya Finca imeeleza kutoa huduma kwa wateja wake ambapo mpaka sasa  watanzania wapatao 800,000  wamepata huduma katika matawi  yake yote yaliyo katika Mikoa 24 nchi nzima.

Finca inafikisha huduma kwa njia ya Mawakala wanaopatika nchi nzima, pia kutoa huduma hiyo ya kifedha kwa njia ya simu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Issa Ngwegwe amesema kuwa wanatoa huduma za kifedha zinazowasidia wateja kuweza kutengeneza biashara ambazo zinawapatia kipato.

Ngwegwe amesema kuwa huduma hizo pia zitawasaidia wateja hao kutengeneza ajira kwa Watanzania wengine wasio katika Sekta Binafsi.

Pia, ameongeza huduma hizo kuwapatia uwezo wa kujitambua na kuwafikisha katika malengo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko wa Benki, Gershom Mpangala amesema kuwa Benki hiyo ina akaunti inayoitwa Mipango Pay Out inayolenga kwa Wastaafu zaidi ambazo zinaweza kumuingizia Mstaafu huyo Riba kubwa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Issa Ngwegwe akizungumza na Waandishi wa Habari  kuhusu utaoaji huduma Benki ya FINCA kwa wateja wake kwenye ofisi zake jijini Dar es Salaam leo
Mkuu wa Masoko wa Benki ya Finca, Gershom Mpangala akizungumzia Mipango Pay Out inayolenga kwa Wastaafu zaidi ambazo zinaweza kumuingizia Mstaafu huyo Riba kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad