HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 10 July 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO

 Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua risiti  ya mmoja wa mama aliyefika kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato aliyekuwa amemleta mtoto wake kupata matibabu.Mhe.Waziri alikua akijiridhisha kama mama huyo amelipishwa fedha katika  matibabu ya mtoto kwakuwa matibabu kwa mtoto chini ya miaka mitato huduma hutolewa bila malipo.
  Waziri Ummy akikagua duka la dawa lililopo kwenye hospitali hiyo (Duka la MSD) ambalo linasaidia upatikanaji wa dawa  katika hospitali hiyo pamoja na vituo vya afya pamoja na zahanati za jirani.Kulia mwisho ni Mbunge wa Jimbo la Chato na naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
 Waziri wa Afya akitoka kutembelea Wodi ya Wazazi iliyopo kwenye Hospitali hiyo,kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Athanasi Ngambakub na katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na madini Dkt.Medard Kalemani
 Waziri Ummy wakijadiliana jambo kwenye jengo jipya linalojengwa la upasuaji,ambapo Waziri ameagiza jengo hilo likikamilika wawape kipaumbele akina mama wajawazito ili kuweza kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi
 Katika wodi waliyolazwa watoto Waziri Ummy akimsalimia mmoja wa mtoto aliyelazwa hospitalini hapo
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimsisitiza jambo Waziri wa Afya wakati wa kuongea na watumishi wa hospitali hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Shabani Ntalambe.
 Dkt.Kalemani akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo(hawapo pichani) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo
 Meneja wa Kanda ya Mwanza wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Victory Sungusia akijibu swali toka kwa Waziri Ummy wakati wa kuongea na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Chato
 Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani)
Picha ya pamoja ya Mawaziri,Viongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo mara baada ya kumaliza ziara. (Picha zote na Wizara ya Afya)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad