HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 10, 2017

KATIKA KUUNGA MKONO SERA YA SERIKALI YA TANZANIA YA VIWANDA ,MANTRAC TANZANIA YAZINDUA MPANGO KUKODISHA NA KUMILIKI MITAMBO

Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.
Hii inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. Alisema katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.Mpango wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.
Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.
Kampuni ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.
Bidhaa zinazouzwa na kampuni ya Mantrac Tanzania zinapatikana katika matawi mbalimbali nchini kama vile Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Mbeya, na Kilimanjaro.Bw Pantaleo alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara kati ya kampuni ya Mantrac Tanzania na wateja kwenye  
mitambo mipya, iliyotumika na kukodisha mitambo, sasa kampuni imeamua kuleta mpango huu wa kukodisha na kumiliki ambapo mteja atalipa kidogo kidogo hadi pale atakapomiliki mtambo wake.Alisema kamupuni ina mitambo mingi inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kutekeleza mpango huu mpya wa kukodisha na kumiliki.Kampuni ya Mantrac Tanzania ndio pekee yenye kibali cha kusambaza na kuuza mitambo mbalimbali inayotengenezwa na kampuni ya CAT hapa nchini Tanzania.
Kampuni pia ina vituo maalum vya huduma kwa ajili ya matengenezo ya mitambo, ina wataalamu wa hali ya juu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa ambavyo hutumika katika kuchunguza tatizo na kutengeneza ubovu unaojitokeza katika mitambo.
Katika mpango huu, vigezo na masharti vitazingatiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad