HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 20 July 2017

WADAU WA KILIMO WAJA MBINU YA KUSAIDIA WAKULIMA WADOGO KUPATA MASOKO YA UHAKIKA

Mkurugenzi Mkazi wa Farm Africa, Steve Ball akizungumza kuhusu umuhimu wa wakulima kupata taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa masoko, wakati wa warsha ya wadau wa mazao ya nafaka iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Mpango mpya unaohamasishwa na wadau wa sekta ya kilimo hatimaye utawapa wakulima wadogo nchini kote fursa ya kupata masoko ya uhakika na endelevu kwa kuepuka madalali wa mazao yao.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Farm Africa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania wa Farm Africa,  Steve Ball alisema kuwa warsha hiyo ililenga kuwafudisha wakulima namna bora kuingia kwenye mfumo rasmi wa biashara ya nafaka.

Alisema kuwa jukwaa hilo la wadau kwenye sekta hiyo linaunganisha biashara nzima ya nafaka kutoka kwenye shamba hadi sokoni  na inashirikisha mkusanyiko wa programu zinazoruhusu watumiaji kusimamia hesabu, mazao ya biashara, soko endelevu na kupata mikopo kutoa kwenye taasisi za fedha.

"Tuko hapa kuzungumza juu ya njia bora ya kuwasaidia wakulima wadogo ili kuepuka madalali wakati wa kutafuta masoko ya mazao yao na ili waweze kupata kwa bei bora zaidi baada ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka juu ya mwenendo wa soko,” alisema.

Aliongeza pia kwamba wadau katika sekta hiyo wana matumaini kwamba wakulima watakusanya nguvu kwa pamoja na kutengeneza maghala yao ya kuhifadhi mazao yao na kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzri zaidi.

Alibainisha kuwa kwa njia ya G-Soko, wakulima wanaweza kuunganisha mavuno yao kupitia ghala lao na kuthibitishwa na kupata huduma za kifedha kwa kutumia nafaka zao kama dhamana. Jukwaa pia hutoa programu ya malipo ya huduma na ukusanyaji wa data wa wakulima.

Alifafanua kamba wadau wanajua kwamba zuio la serikali kuuza chakula ni kudhibiti hali ya uchumi wa nchini na vile vile kuzuia kununua unga, mchele kutoka nje baada ya wakulima kuuza mahindi na mtama lakini aliongeza ni muhimu kwa serikali kuwajengea wakulima uwezo ili kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula hapa hapa nchini.

Kwa upande wake, Mshauri wa Sera kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Revelian Ngaiza alisema kuwa serikali inatafuta njia bora ya kupunguza gharama za shughuli za kilimo kwa mkulima mdogo kwa kuboresha mfumo wa miundombinu, usafiri na usambazaji.

"Kuboresha upatikanaji wa habari kwa wakulima wadogo juu ya bei ya soko na mahitaji ya walaji na kuwezesha ushirikiano na sekta binafsi na serikali katika kumuinua mkulima mdogo vijijini,’ alisema.

Alisema serikali ina nia ya kuanzisha mikakati na sera mbalimbali za kubadilisha kilimo ili kuendeleza utendaji bora na uboreshaji ulioimarishwa na ukuaji wa uchumi.

"Katika Tanzania peke yake, karibu asilimia  40 nafaka hupotea kutokana na uhifadhi duni na mabadiliko ya hali ya hewa kila mwaka, kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 332 na kuacha wakulima wa nafaka kwenye hasara kubwa," alisisitiza

Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Mipango ya Maendeleo Mjini na Vijijini (RUDI), Afisa Mtendaji Mkuu wake, Lameck Kikoka ana matumaini kuwa kuingilia kati kwa wadau hao wa kilimo nchini na mashirika ya kimataifa ya kilimo kutasaidia wakulima zaidi ya 30,000 nchini Tanzania pekee kupata masoko zaidi, hivyo kupambana na umaskini na kuboresha ustawi wa wakulima.

Alisema kuwa zamani changamoto za wakulima zilikuwa kubwa gharama kubwa za pembejeo kama vile mbegu zilizoboreshwa na mbolea na wengi walikuwa hawana mahali pa kuhifadhi mazao yao wakati wanasubiri bei bora kwenye soko.

"Lakini kuingilia kati kwa serikali na kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kutaendelea kuwahahikishia wakulima bei bora na usalama wa mazao yao na soko endelevu kwa mazao yao wakati na kuongeza uwezo wao wa kuhifadhi kwa kuendelea kujenga maghala yao wenyewe yatakayo thibitishwa na serikali,” alifafanua.

"Ili kusaidia wakulima kufaidika na fursa hizi, Farm Africa na washirika wa ushirika (RUDI) sasa wanataka kusaidia wadogo wa Tanzania na Uganda kushika mchele, mazao na maharage ya ziada."

"Tunapaswa kulima  na kuvuna zaidi baada y kupata uelewa wa mfumo rasmi wa biashara ya nafaka na uelewa wa kupata soko la uhakika bila madalali ," alisema Emerita Singaile.  Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima wa Makalali kutoka mkoani Iringa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad