HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 17 July 2017

USIKOSE UZINDUZI WA ALBAMU YA JERUSALEM CITY SINGERS MWANZA

Uzinduzi wa albamu ya tatu kutoka kwaya ya JERUSALEM CITY SINGERS ya Bugarika Jijini Mwanza, unatarajiwa kufanyika jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza. Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Samwel Maneno amesema hakuna kiingilio katika uzinduzi huo na kwamba shughuli nzima itaanza majira ya saa saba kamili mchana ambapo waimbaji mbalimbali wakiwemo Born To Praise, Voice Of Calvary na Lake Zone watahudumu siku hiyo. 

 "Hii ni albamu yetu ya tatu ya video iitwayo MUNGU WA AJABU ambapo imetanguliwa na albamu mbili ambazo ni DUNIA MAHUTUTI na HAJAKUSAHAU hivyo nawakaribisha watu wote kushiriki nasi kwenye uzinduzi huo". Amesema Maneno. Usikose uzinduzi huu, ni Jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza, kuanzia saa saba kamili mchana, ambapo hakuna kiingilio. Wasiliana na Jerusalem City Singers 0758 06 10 44
Bonyeza HAPA taarifa zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad