HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 20, 2017

TUNDU LISSU AKAMATWA AKIWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA KWENDA RWANDA

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu  Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kinachoanza kesho.

Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.

Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad