HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 3, 2017

TIMU NNE ZATINGA HATUA YA NUSU FAINALI SPRITE BBALL KINGS


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi katika uwanja wa chuo kikuu cha Dar es salaam, ikiwa ni hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na The fighter na timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41 za The fighter .

Mechi ya pili iliwakutanisha Flying dribblers ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 91 dhidi ya Osterbay aliyepata vikapu 82, TMT wakaumana na Dream chaser na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 96 dhidi ya vikapu 73.

Mechi ya nne iliyowakutanisha Kurasini Heat na Kigamboni Heroes ilimalizika kwa vikapu 64 vya Kurasini Heat dhidi ya 59 vya Kigamboni Heroes. 

Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za Robo fainali na kupatikana kwa timu nne zitakazoendelea kwenye hatua ya nusu fainali kutachezeshwa kwa droo maalumu kwa ajili ya kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano haya ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017.

"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki hii ndizo zilizofanikiwa kuendelea katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Sprite Bball kings 2017 "amesema Basilisa.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha shiling milion 15.

Timu ya The fighter (jezi nyeupe) ikisalimiana na timu ya Mchenga (jezi nyeusi) wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kushinda kwa vikapu 109 dhidi ya vikapu 41
Mchezaji wa timu ya The Fighter akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Mchenga  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41.

Mchezaji wa timu ya kikapu ya TMT  akipiga pigo la adhabu kwa upande wa timu yake wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Dream Chaser  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya TMT  kuibuka na ushindi wa vikapu 96 dhidi ya 73.
 Timu ya Dream Chaser  (jezi nyeupe) na TMT (Jezi buluu) wakikaguliwa na waamuzi wa mchezo huo kabla ya  kuanza kwa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad