HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 July 2017

FC VITO KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA KESHO


Msafara wa wachezaji, makocha na walezi wa timu ya vijana ya FC Vito ya Lindi, umetua salama jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabidhiwa bendera ya Taifa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

FC Vito inatarajia kuondoka nchini Julai 5, kwenda Helsinki, Finland kushiriki michuano ya vijana ya Helsinki Cup 2017, michuano ya nne kwa ukubwa barani Ulaya kwa vijana

Kikosi hicho kitakabidhiwa Bendera ya Taifa hapo kesho katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ubalozi wa Finland makutano ya mitaa ya Mirambo na Garden Avenue jijini Dar es Salaam....

Mgeni rasmi wa hafla hiyo, ambaye ndiye atakayekabaidhi bendera ya taifa ni Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja...No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad