MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (CCM) ametimiza kwa vitendo ahadi yake ya kuwawezesha kiuchumi wanawake ambao ni wafuasi wa CCM kwa kukusanya zaidi ya Sh35 milioni ambazo wanawake hao walioko kwenye vikundi vya ujasiriamali watapatiwa mtaji wa kiasi cha Sh320,000 kwa kila kikundi.
Kati ya fedha hizo, Sh 20 milioni zilitolewa na Shonza huku wadau wanaomuunga mkono mbunge huyo wakitoa zaidi ya Sh15 milioni katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM kiuchimi ambao ulizinduliwa rasmi juzi na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson.
Akizungumzia mradi wa uanzishwaji wa mfuko huo, Shonza alisema moja ya ahadi zake wakati wa kampeni za kuomba ridha ya kuchaguliwa na wanawake mwaka 2015, aliwahakikishia kuwainua kiuchumi na baada ya kuchaguliwa alianza na utaratibu wa kukutana wanawake kwa kila kata kwa ajili ya kuunda vikundi, kuvisajili ili viweze kukopesheka.
Naibu
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza wakipanga vizuri kitita cha fedha
kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya kutunisha mfuko
wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za
ujasiriamali kupitia vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi
na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo
alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge
huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320,000 kutoka Kata zote 100 za
Mkoa wa Songwe.
“Tayari kuna kikundi kwa kila kila kata ambavyo nilivisimamia mimi kuanzia kupta usajili na vingine vimeanza kazi za ujasiriamali na vina vifanya kazi, kwa kila kikundi niliahidi kuwasaidia Sh200, 000 kama mtaji wa kuanzisha shughuli yoyote ya ujuasiamali, lakini nikaone niwakutanishe wadau wengine watakaoniunga mkono kwenye hili na nashukuru mmeonesha ukweli wenu”.
Alisema wanawake wa Songwe hawahitaji kutafutiwa kazi maofini, kwani ni wachapa kazi lakini changamoto waliyo nayo ni mitaji tu kwani uwezo wa kuingia shamba na kuanzisha mradi wowote wa kiujasiriamali wanao.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Tulia aliwataka wabunge wa viti maalum nchini kwenda kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wakipigiwa kura badala ya kuwatelekeza kwa kisingizio cha kutokuwa na majimbo.
Naibu
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (katikati) wakiwa wamekumbatia
kitita cha fedha kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya
kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha
shughuli za ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa
rasmi juzi na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na
Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau
wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320, 000 kutoka Kata
zote 100 za Mkoa wa Songwe.
Alisema jambo lililofanywa na Shonza ni mfano tosha na kudhihiridha kwamba anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM n azma ya Serikali ya kufikia nchi ya viwanda.
Katika uzinduzi, huo, Mbunge Shonza aliungwa mkono na wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Jimbo la Mtama, Livingstone Lusinde ‘Kibajaji’, Mbunge wa Jimbo la Pangani Tanga, Jumaa Awesu, Janeth Mbene wa Ileje na Josephat Hasunga wa wa Jimbo la Vwawa Mbozi
Wabunge
wakicheza muziki na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Songwe, waliofika
kwenye harambee ya uzinduzi wa harambee ya kutunisha mfuko wa
uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za
ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko
huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni
zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa
Sh320, 000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe.
No comments:
Post a Comment