HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 16 July 2017

FEZA SEKONDARI YATOA ALIYEONGOZA KITAIFA KWA WAVULANA KIDATO CHA SITA KATIKA MASOMO YA SANAA

 Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza akiwa amebebwa juu na wanafunzi wenzie wa shule hiyo baada ya kuibuka Mwanafunzi bora kitaifa katika Masomo ya Sanaa ya Biashara katika matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani Julai 15, 2017.
  Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza  akiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake wote wawili ,Thomas Samky na Victoria Samky walipofika shuleni hapo
 Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mitihani ya Kidato cha sita na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa, Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo wakiwa ni wenye furaha kufuatia matokeo kutoka ambapo Atuganile amekuwa wa tatu kitaifa katika Masomo ya Sayansi na Kabhabhira amekuwa wa Saba katika masomo hayo.
 Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo wakilakiwa na walimu wao baada ya kuwasili shule hapo.
 Mwanafunzi aliyefanya vizuri na kuwa wa tatu  katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,  Atuganile Cairo akiwa na Mama yake Mzazi  akimpongeza kwa kufanya vizuri katika mtihani huo wa kidato cha Sita
 Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo  wakisalimiana na Mwalimu mkuu wa Shule ya Wasichana fedha ,Ibrahim Rashid pamoja na baba yake atuganile Jimmy Cairo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad