HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 25 July 2017

RATIBA YA NDONDO CUP, WATANGAZAJI CLOUDS WAGAWIANA TIMU


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

ROBO fainali ya Ndondo Cup inaendelea tena siku ya Alhamisi kwa timu nane kuumana katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Kinesi.

Droo hiyo iliyochezeshwa jana na kila timu kufahamu anapambana na nani katika hatua ya robo iliweza kuwa ya aina yake baada ya watangazaji wa vipindi mbalimbali wa Clouds kugawana timu hizo na kuwapa ahadi lukuki .

Hii ndo Ratiba ya Robo fainali

Alhamis 27/07/2017

Vijana Rangers vs Kibada one 

Ijumaa Tar 28/07/2017

Goms United vs Mlalakuwa Rangers 

Jumamosi Tar 29/07/2017

Mpakani Combine vs Misosi Fc 


Jumapili Tar 30/07/2017

Keko Fanicha vs Stimutosha Fc

Leo tena wenyewe wamebaki na timu yao Mlalakuwa Rangers, kwa hiyo hawakuwepo kwenye draw ya kila kipindi kupata timu yake. XXL wao timu yao ni Keko Furniture, Jahazi wenyewe wameangukia kwa Mpakani Kombaini, Clouds 360 timu yao ni Misosi FC wakati amplifier watakuwa na Vijana Rangers, Kibada One wameangukia kwa Power Breakfast huku Goms United wakitua kwa Shilawadu na Stim Tosha ikienda kwa wazee wa Alasiri.

Baada ya droo hiyo kila kipindi kilitoa ahadi na mbwembwe kibao na kuziahidi timu hizo kuwa watanunua kila goli huku kipindi cha 360 wakitoa ahadi ya kuwapeleka mbuga za wanyama iwapo watakuwa mabingwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad