Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
(wapili kushoto) akioneshwa ramani ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na
ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia
maji na hatua iliyofikiwa
katika utekelezaji wake wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe
akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua hatua iliyofikiwa
katika mradi wa ukarabati na upanuzi wa mtambo wa maji chalinze na
ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia
maji. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa
Mazingira Chalinze (CHALIWASA)Mhandisi Christer Mchomba na kushoto ni
Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya WAPCO inayotekeleza mradi
huo.
Mafundi wakiendelea na Kazi ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhi na
kusambaza maji katika Jimbo la Chalinze.
Baadhi ya mitambo ikiwa katika moja ya maeneo unakotekelezwa
mradi huo utakaonufaisha wakazi wa Jimbo la chalinze na sehemu ya
Wilaya ya Handeni.
Sehemu ya mabomba yakiwa katika moja ya maeneo
unakotekelezwa mradi huo.
No comments:
Post a Comment