HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 8, 2017

Naibu Waziri Ole Nasha awasaa watanzania kula korosho

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha amewaasa watanzania kula korosho kwa wingi ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanagharimu na kukosa nguvu kazi ya taifa.

Nasha ameyasema leo katika Siku ya Korosho katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), amesema kuwa korosho inasaidia kuepukana na mafuta mwilini ambayo yanasababisha magojwa ya moyo kwa kiasi kikubwa.

Nasha amesema kuwa kilimo cha korosho kimeboreshwa na kuwataka wakulima kulima mbegu za kisasa pamoja na kufuata ushauri wa watalaam wa kilimo katika maeneo yao.

Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo watu watumie fursa ya kujifunza kilimo cha kurosho katika kujenga uchumi wa viwanda wa adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Magufuli.

Makamu Mwenyekiti Bodi ya Korosho, Makola Majogo amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ulimaji wa kilimo cha kisasa cha kurosho ili  zao hili kuleta maendeleo uchumi wa nchi pamoja na mkulima kunufaika na kilimo hicho.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akizungumza katika siku ya Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Korosho, Makola Majogo akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wa zao la korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na mifuko ya korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wa waliofika katika Siku Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad