HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 8, 2017

KAMPUNI YA HUSEA YAZINDUA MPANGO WA UPIMAJI NA UPANGAJI WA MAKAZI RASMI KATA YA MSIGANI - MBEZI WILAYA YA UBUNGO - DAR

Mwenyekiti wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Renny Chiwa akitoa maelezo machache juu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' katika uzinduzi wa uliofanyika Kata ya Msigani-Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Bw. Chiwa alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia juhudi za serikali za kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini nzima na pia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania kupitia ushauri na utoaji elimu kwa wananchi katika masuala yote ya ardhu kwa nia ya kutengeneza makazi bora yaliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.
Mkurugenzi wa Upangaji wa Vijiji na Miji kutoka Wizara ya Ardhi na Makazi, John Lupala, alisema ili kufanikisha mradi huo kwa haraka atapangwa Ofisa Ufuatiliaji kutoka wizarani ashirikiane na HUSEA katika mradi huo wa Kata ya Msigani, Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Diwani wa Kata ya Msigani Wananchi walijitokeza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Pamela Maro akiwafafanua machache mbele ya waandishi wa habari juu ya Mradi wa 'Ardhi Clinic' katika uzinduzi uliofanyika katika Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa malengo makuu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' ni tiba mbadala kwa changamoto mbali mbali za masuala ya ardhi baada ya kugundua kuwa changamoto nyingi zinatokana na masuala ua ardhi hapa Tanzania kama migogoro ya wafugaji na wakulima, wananchi kuuziwa maeneo ya wazi, utapelikwenye masuala ya ardhi, uendelezaji wa makazi usiofuata mipango, ukosefu wa maadili katika taaluma za upangaji na upimaji, ukosefu wa hati miliki, ukosefu wa huduma za jamii n.k hazina tofauti na magonjwa ambayo wanahitaji tiba haraka kuyakabili.
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya ardhi. Diwani wa Kata ya Msigani, Israel Mushi alisema kuwa upimaji huo utasaidia serikali kupata mapato yake stahiki pindi utakapokamilika na kwamba utasaidia kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa migogoro ya ardhi ndani ya kata hiyo.
Vifaa vya kisasa vinavyotumika katika upimaji wa ardhi.
Mwenyekiti wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Renny Chiwa akiwashukuru waandishi wa habari jinsi walivyojitokeza kuungana nao katika uzinduzi wa Mradi wa 'Ardhi Clinic' unaowapatia fulsa wananchi wa Kata ya Msigani-Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam kupimiwa na kupangiwa makazi yao.
Mfanyakazi wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA) akitoa maelezo kwa wananchi waliofika katika uzinduzi wa mradi wa 'Ardhi Clinic' uliofanyika katika Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad