HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 25 July 2017

MSUVA AAGA RASMI LEO, YANGA WASHAMALIZANA NA DIFAA HASSAN ELJADIDI YA MOROCCO


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten


Na Agness Francis, Globu ya Jamii.


Winga machachari wa timu ya Yanga Simon Msuva anatarajiwa kuondoka kuelel]kea nchini Morocco kwa ajili ya vipimo ili kujiunga na timu ya ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC) inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mchezaji Saimon Msuva anatarajia kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya zoezi la vipimo vya afya ili kukamilisha mchakato mzima wa usajili wa mchezaji huyo katika timu ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC).

Ten amesema kuwa, walishamaliza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kujiunga nao na wamempa baraka zote kijana wao kwa ajili ya kuanza maisha mapya ya soka nchini Morocco.

Timu hiyo iliyomaliza msimu uliopita huku ilishikilia nafasi ya pili katika nmsimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 59, huku WCA Casablanca wakiwa kilelelni kwa point 66 ligi kuu ya morocco, Ambayo inajumuisha timu 16 kama ilivyo ligi kuu ya Tanzania bara. 

Hata hivyo uongozi wa yanga unasubiri majibu ya vipimo vya Msuva na kuendelea na taratibu zote za kuuzwa kwa mchezaji huyo ambaye ameitumikia club hiyo misimu 5 akiwa kiungo mshambuliaji mwenye jezi namba 27.

Mapema mchana huu Msuva ameenda klabu ya Yanga kwa ajili ya kuaga na kupata baraka za viongozi wake waliokuwa nae katika maisha ya soka ndani ya Klabu ya Yanga kwa miaka mitano.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad