HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 17, 2017

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,  Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja  na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan.  Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza  Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,  Dk. Jane Goodall.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa  Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,  Dk. Jane Goodall.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,  Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja  na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan.  Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Dk. Jane Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika Ujumbe wake Dk. Goodall aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija Simba ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na watendaji wengine wa Taasisi hiyo.
Katika mazungumzo yao Dk. Goodall pamoja na mambo mengine amezungumzia uharibifu wa shoroba za wanyama pamoja na makazi yao katika hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe. Alisema kwa sasa hifadhi hiyo imezungukwa na maakazi ya binadamu hali iliyosababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.
Aidha Dk. Goodall alimuelezea Makamu wa Rais jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Gombe ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora ya matumizi ya ardhi.
“inawezekana tatizo kubwa linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na uelewa mdogo wa wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma. Kwa sasa wananchi kutoka katika  vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma wanapatiwa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya shilingi Milioni 400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili kujiwezesha kiuchumi na kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan yenye leno la kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii imeanza kuleta mafanikio.
Dk. Goodall ametaja changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa  hushiriki katika shughuli ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama vile kilimo na ufugaji usio endelevu.
Kwa upande wake Makamu wa Rais alisema serikali inafanya kazi kubwa katika kuhakikisha mazingira ya hifadhi za Taifa pamoja na ikolojia yake yanatunzwa. Makamu wa Rais amemhakikishia Dk. Goodall kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakiksha wananchi wanafanya shughuli za kujiletea maendeleo bila kuharibu mazingira. “Ni muhimu kuishirikisha jamii inayoishi pembezoni mwa hifadhi zetu katika suala la uhifadhi wa mazingira lakini pia kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi”, alisema Makamu wa Rais. Kuhusu suala la wakimbizi kuharibu mazingira, Makamu wa Rais aliahidi kutoa maelekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona namna bora ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Mwisho, Makamu wa Rais alimpongeza Dk. Goodall kwa kupewa tuzo ya heshima na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama ishara ya kutambua mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa Sokwe na mazingira kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad