HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 17 July 2017

YANGA YATEUA WAJUMBE WAPYA WATATU WA KAMATI YA UTENDAJI

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umejaza nafasi zilizoachwa wazi kwa mujibu wa katiba ibara ya 28:(1)d  ikiwa ni maazimio ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa tarehe 15/7/2017.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga kimeweza kufikia maazimio hayo kutokana na ibara hiyo anakuwa na mamlaka ya kujaza nafasi zile zilizoachwa wazi na wajumbe wa kamati.

Kikao hicho kimeweza kuwateua wajumbe watatu ambao ni Mohamed Nyenge, Tonny Mark na Majid Suleiman ambao wataanza majukumu yao yataanza moja kwa moja wakichukua nafasi za wajumbe wawili walioamua kujiweka pembeni pamoja na  mjumbe aliekuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano Mhandisi Malume aliekwenda nje ya nchi kwaajili ya masomo.

Pamoja na hilo, uongozi wa Yanga mapema wiki hii iliweza kukutana na kufanya kikao na wachezaji wa zamani wa timu hiyo na kufikia maazimio mbalimbali yenye malengo ya kuisaidia timu yao na kushirikiana nao bega kwa bega.
Maazimio hayo ni :

1.Kuwashirikisha katika masuala ya klabu na kuwaweka karibu na klabu.

2.Kujenga umoja wa wana Yanga kwa ujumla.

3.Kuunda safu ya uongozi wao itakayorahisisha mawasiliano baina yao na uongozi wa klabu.

4.Kuweka kumbu kumbu kwaajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wao.

5.Kusaidiana katika suala zima la ugunduzi wa vipaji vya wachezaji kwa manufaa ya klabu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad