Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiwa ameongozana na kamati ya fedha wakikangua barabara ya Saranga, King'ong'o ambazo zipo kwenye Matengenezo ya dharura, jijini Dar es Salaam.
Dereva wa pikipiki akikwepa shimo katika barabra ya Saranga, King'ong'o jijini Dar es Salaam.
Halmashauri ya manispaa ya Ubungo, kupitia ziara ya kamati ya fedha iliyokuwa ikiongozwa na Mstahiki Meya, Boniface Jacob walifika kujionea hali ya uharibifu wa barabara hasa maeneo ya Kwandevu kuelekea King'ong'o kata ya Saranga
Nakuhaidi kuishughulikia kwa dharula maeneo mawili
yaliyoonekana kuharibika sana na kisababisha uharibifu wa magari, foleni na kuhatarisha Maisha ya watembea kwa miguu.
Matengenezo ya dharula yataanza hivi karibuni chini ya Mhandisi wa Halamshauri ya Ubungo huku Manispaa ikiendelea kufuatilia kuingiziwa fedha za barabara hiyo kutoka Manispaa ya kinondoni kwenye akaunti ya pamoja iliyofungwa na Bodi ya barabar ambapo zilitengewa kiasi cha shillingi Millioni 400 kuweka zege maeneo yote ya miteremko na vilima vya Matosa mpaka kimara kupitia King'ong'o.
IMETOLEWA Na OFISI YA MSTAHIKI MEYA HALMASHAURI YA MANISPAA UBUNGO.
No comments:
Post a Comment