HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 9, 2017

YANGA KATIKA LIGI NA BAADA YA LIGI.

Honorius Mpangala

Moja ya misemo ya kiswahili inayopendwa kutumuwa na watanzania ni "usijisifie una mbio bali msifie na anayekukimbiza" msemo huu ungekuwa bora sana kuwa elezea klabu ya Simba kuwa walikua vyema msimu tofauti na msimu uliopita.

Msimu wa 2016/17 kwa upande wa klabu ya Yanga unaweza kusema ulikua mgumu sana na huenda ungewanyima taji kama tu wasingechukua maamuzi magumu baada ya kuona watu wanapangwa katika kikosi kwa mazoea,binafsi naamini taji la Yanga ni kwa marekebisho makubwa yaliyofanyika na Kocha George Lwandamina.

Tathimini yangu kwa msimu mzima kwa klabu ya Yanga.

Moja ilianza ligi ilikuwa na mchoko wa hali ya juu baada ya kuumaliza mwaka mzima wa kalenda wa 2016 kwa kufululiza kucheza mechi ikiwa ni kitu ambacho haikuzoeleka kwa wachezaji wake.

Mbili kiburi cha kujiona wakimataifa  kulisababisha Yanga iweza kuona michezo kama dhidi ya Stands Utd, Ndanda, Mbeya City kuwa migumu kwao tofauti na ilivyokua msimu uliopita.

Tatu,klabu ya yanga kukumbwa na changamoto ya mishahara ilikua ni moja ya sababu iliyowafanya wachezaji kukutwa na visununu kama Yale yaliyotokea kwa Vincent bossou aliyekuja kutofautiana na uongozi kwasababu ya malipo ya mshahara wake kama ilivyokua kwa Obrey Chirwa.

Majeruhi ya key player kama Juma Abdul, Donald Ngoma,Thaban Kamusoko, Amis Tambwe kwa nyakati tofauti watu waliochukua nafasi zao hawakuweza kuwa fit na kuisaidia klabu kucheza kwa kasi na kiwango kama cha waliopata majeruhi.

Nne, Matatizo ya Mwenyekiti wa klabu kulimfanya kukaa mbali na kushindwa kuwa karibu na wachezaji ambao waliamini uwepo wake katika kuwasapoti kulitoa hamasa kubwa kwao.

Tano, kuna haja kubwa ya kuandaa mikakati ya kuweza kufanikiwa katika michezo ya kimataifa kwani japo msimu uliopita timu iliishia hatua ya robo fainali ila mapungufu yalikuwa mengi kwasababu ya maandalizi ya klabu katika kuwakabili wapinzani wao.
Yanga ilijikuta inakuwa na wakati mgumu kushinda mechi za nyumbani kutokana na mikakati midogo waliyokua wakiianda.

Mikakati iliyotakiwa kuifanikishia Yanga ilitakiwa kuwa na ushirikiano na TFF lakini  kwa kipindi kirefu hawakuweza kuwa kitu kimoja Mara baada tu ya Yale maneno ya Jerry Muro aliyokua akiilalamikia TFF.

Kwa upande wa yanga baada ya ligi ifanye nini kwa msimu ujao ni haya.

Eneo kubwa ambalo Yanga imekuwa na changamoto ni watu mbadala wa kikosi kinachoanza. Kikosi cha yanga kikianza halafu ukatazama waliopo ktk benchi unaona uwiano haupo kwani,kama ngoma anaanza halafu benchi yuko Anthony matheo au malimi busungu je unategemea nini kama kazi aliyoishindwa ngoma ataiweza matheo?.

Yanga ilikua na kikosi kipana lakini kilikua hakina uwiano wa viwango vyao. Sehemu ya beki ilikua vyema chini ya waandamizi  Cannavaro,Bossou na Yondani huku Dante na Ngonyani wakiwa ni watu wanaojifunza toka kwao.

Sehemu ya kiungo ya Yanga hadi leo wanahangaika kuziba pengo la Athumani Idd Chuji na Frank Domayo, kwa imani niliyonayo kwa uwezo aliokua nao Kamusoko msimu wake wa kwanza ndani ya yanga ndiyo angemkuta Chuji yule wa pasi manati ya mzungu,Chuji wa pasi rula nafikiri tungeweza kuona utamu Mara dufu.

Maeneo ambayo Yanga wanatakiwa kuyafanyia kazi ni kumpada DM ( defensive midfielder) wa maana atakayeweza kusaidiana na hawa wazawa kama Juma Saidi Makapu na sio kumtegemea Justine Zulu ambaye namwona kasi inamwacha nje kutokana na kuwa na umri mkubwa.

Sehemu ya mshambuliaji wa kati wanatakiwa watu wenye kupambana na kutaka kuisaidia timu na wao wenyewe,mfano kwa ligi yetu na kwa wachezaji wa ndani kuna washambuliaji wapambanaji ambao wakipewa nafasi katika klabu wanaweza kuwa msaada. Unaweza kuona tofauti kati ya Mateo Antony na Kelvin Sabato kiduku wa Majimaji jamaa ni mpambanaji wa kweli kama ilivyokua kwa Abdulrahman Musa wa Ruvu shooting.

Pia wanaweza kutazama kwa kwa nafasi ya walinzi wa kati kati ambao ni wazawa ambao bila kupepesa macho beki kama Nurdin Chona na mwenzake Mwashota ni kati ya walinzi wagumu wa aina ya soka la shoka kama achezalo Yondani.

Kama itatokea nafasi kwa beki toka nje basi wangeweza kumtazama vizuri Asante Kwasi wa Mbao Fc ambapo binafsi namwona beki mnyama kwelikweli katika uwanja.

Sina shaka na nafasi za mawinga au fullbacks kwani upande wa kulia kuna watu bora kabisa ila mtu pekee ambaye anahitajika kutafutiwa msaidizi wake ni nafasi ya beki ya kushoto.

Mwinyi Haji Mngwali ni moja ya mabeki bora wa kushoto lakinichangamoto inakuja pale anapokuwa na majeruhi au tatizo la kadi unajiuliza ni nani aliyesahihi kumsaidia.Kunahitajika nafasi ya beki wa kushoto ambaye binafsi nimemfuatilia vyema fullback ya kushoto ya mbao Jamal mwambeleko anajiamini na anauwezo kucheza wingback vyema huku akiwa na jicho la utoaji mzuri wa pasi kwa wafungaji.

Kwa eneo la beki nafikiri ni suala la kuwaamini tu yule Pato Ngonyani ni mnyama sana ila bahati hana, kiungo cha kati kuna  Salmin Idd Hoza wa Mbao, kuna kiungo mwingine wa chini ambaye anauwezo mzuri ni yule Ally Makarani wa Mtibwa Sugar ambaye ana staili kama za Mzamiru Yasin wa Simba anacheza 6,8 kwa usahihi.

Wako wachezaji wengi lakini kwa wale walioshiriki ligi ya Vodacom wangeweza kuanza na hao kabla ya kuwafuatilia kina Meshack Chaila toka Zesco kama zilivyotetesi za klabu ya Yanga zinavyokwenda.

Kabla hawajafikiria kuhusu mkataba wa Donald ngoma wangeanza na kuhakikisha wanambakisha klabuni na sio kuondoka. Kwanini natetea Ngoma kubaki, nafikiri kila mmoja anamkumbuka Kpah Sherman alikua moja ya washambuliaji niliowakubali kwa uwezo wake wa kuficha vyema Mpira lakini alikua mwoga kwa beki aina serge paschal wawa.

Mtu pekee ambaye alikua anampa shida Sergio Wawa katika ligi ya vodacom ni Ngoma aliweza kumpindua atakavyo aliweza kucheza nae kwa ubavu vyema. Kama ujuavyo sio rahisi kufunga magoli mbele ya Wawa na Agrey Morris lakini alikua anapinduka hata acrobatic mbele yao na kufunga. Unapotaka kumlaumu Ngoma kuhusu uwajibikaji wake ndani ya yanga tunapaswa na kufahamu kuwa kazi ya wachezaji ni kucheza na kulipwa kimoja kikilega kinatoa matokeo hasi kwa klabu.

Katika nafasi ya makipa ningewashauri yanga wangeachana na Juma Pondamali na kutafuta kocha wa makipa toka Kenya ambako naamini wana makocha bora wa makipa, nalisema hili kwa kurejea kile kikichotokea kwa ivo mapunda alipoenda kucheza ligi ya Kenya alivyobadilika.

Ni hayo tu ambayo nimeweza kuitazama yanga msimu huu na kupendekeza nini kifanyike huku benchi likibaki kama lilivyo.

Mido sankala pasi mpapaso.0628994409

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad