HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 1, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AFURAHISHWA NA UJIO WA TIMU YA LIGI KUU UINGEREZA EVERTON

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KLABU ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza itashuka dimbani Julai 13 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup.

Everton ambayo ni mshirika mkubwa wa kampuni ya SportPesa itakuja chini ikiwa na kikosi kizima kinacho nolewa na kocha raia wa Uholanzi Ronald Koeman katika mchezo huo ambao pia wataumia kama maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Robert Elston alisema mchezo huo utatumiwa na kocha wao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huku akijivunia kuwa timu ya kwanza inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kucheza na timu kutoka Afrika Mashariki.

"Kocha Ronald Koeman na wachezaji wake watautumia mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na pia wanategemea mchezo mzuri," alisema Elston.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema ujio wa klabu hiyo utakuwa msaada mkubwa kwa klabu za Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Everon.

"Ujio wa Everton nchini utakuwa na faida kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwakua zitajifunza moja kwa moja kuhusu masuala mbalimbali ya kiutawala na kiufundi," alisema Dk Mwakyembe.

Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza Juni 5 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ikishirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambazo ni Simba, Yanga, Singida United, Jang'ombe Boys, Nakuru All Stars, Tusker, Gor Mahia na AFC Leopards.

Waziei wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harisson Mwakeyembe akizungumza na waandishi wa habati wakati wa utambulisho wa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Everton Robert Eliston (Kulia) pia pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup utakaofanyika Julai 13 mwaka huu
Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Everton Robert Eliston akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wao wa nchini Tanzania pamoja na  mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup utakaofanyika Julai 13 mwaka huu.Kulia ni Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton Leon Osman na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Pavel Slavkov.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad