HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 June 2017

Dkt. Kyaruzi aikabidhi majukumu Bodi mpya ya TGDC

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Dkt. Dkt. Alexander Kyaruzi akitoa maelekezo wakati wa kuikabidhi rasmi majukumu bodi mpya ya TGDC. 

Na Johary Kachwamba -TGDC
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi amezindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi nchini (TGDC) na kuipa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. TGDC ni kampuni tanzu ya TANESCO

Uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Ofisi za TGDC na kuhudhuriwa na wajumbe wa menejimenti ya kampuni hiyo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo Dkt. Kyaruzi alisema kulingana na majukumu ya TGDC waliona ni vyema wachague Wakurugenzi wenye taaluma tofauti ili kuisaidia kampuni katika nyanja mbalimbali.

“Tuliona kwa shughuli za uendelezaji geothermal basi tutafute mtaalam wa jioloiia, tukamteua Dkt. Mshiu, Uhandisi Dkt. Mwinuka na mtaalam wa mambo ya fedha Ndugu. Segeja” alisema Dkt. Kyaruzi.

Akizungumza Kaimu Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi. Kato Kabaka alimshukuru Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya TANESCO kwa uteuzi huo, na kuahidi kuipatia Bodi ushirikiano kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu.

Naye Mwenyekiti mteule wa Bodi ya TGDC, Ndugu. Beatus Segeja alieleza watashirikiana vyema kwa kutumia taaluma zao kutimiza majukumu waliyokabidhiwa ya kuisimamia TGDC.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGDC, Ndugu, Beatus Segeja anaongoza wajumbe wengine wawili ambao ni Dkt. Tito Mwinuka na Dkt. Elisante Mshiu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad