Mratibu wa kampeni ya kitaifa Bw. Anyitike
Mwakitalima akizungumza wakati wa mkutano kujadili uhusiano kati ya usafi wa
mazingira na lishe bora kwa watoto jijini Dar es Salaam juzi.
Dkt Generose Mulokozi (kulia) kutoka shirika la IMA
World Health akisema ‘Nipo Tayari’ kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa
mazingira kwa lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu
yanayogharimu maisha ya Watanzania.
Mtaalamu wa lishe wa Unicef Mauro Brero akitoa
ishara ya kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira yenye kauli
mbiu ya Nipo Tayari ikiwa na lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile
kipindupindu yanayogharimu maisha ya Watanzania.
.Washirika
wa maendeleo nchini wamekutana jijini Dar es Salaam leo kujadili,
pamoja na mambo mengine, umuhimu wa usafi wa mazingira katika lishe bora
kwa watoto na kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira
yenye kauli mbiu ya “Nipo Tayari”.
Kampeni hiyo inayoratibiwa na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia, Wazee na Watoto imejikita
katika kuhamasisha watu, mijini na vijijini, kujenga utamaduni wa kuwa
na vyoo na kuvitumia kikamilifu na kunawa mikono na sabuni mara baada ya
kutoka chooni.
“Bila kuzingatia usafi wa mazingira, lishe bora
kwa mtoto inaweza kuathiriwa na magonjwa ya kuhara kama vile
kipindupindu, hivyo kuondoa virutubisho vyote mwilini. Ndio maana usafi
wa mazingira na lishe bora kwa watoto ni vitu vinavyotakiwa kwenda
pamoja”, anasema Dkt Generose Mulokozi kutoka shirika la IMA World
Health.
Akizungumza katika mkutano huo, Mratibu wa kampeni hiyo
ya kitaifa Bw. Anyitike Mwakitalima alisema: “Mazingira machafu na
ukosefu wa vyoo umethibitika kuwa chanzo kikubwa kinachosababisha
kudumaa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu zinaonyesha
kwamba asilimia 34 ya watoto wa umri huo nchini wamedumaa kutokana na
kuishi katika mazingira yasiyokuwa na vyoo na kutozingatia kanuni za
afya.
Alisema kuwa ukosefu wa lise bora pia hupunguza kinga ya
mwili kwa watoto hivyo kuugua mara kwa mara na kuwafanya kushindwa kukua
vizuri kimwili na kiakili.
Utafiti wa afya uliofanywa nchini
Tanzania 2015-16 umeonyesha mafanikio ambapo namba ya watoto waliodumaa
imepungua hadi asilimia 34 ikilinganishwa na mwaka 1992 wakati nusu ya
watoto walikuwa wamedumaa.
Utafiti mwingine uliofanyika nchini
hivi karibuni umeonyesha kuwa madhara ya udumavu kwa watoto hauishii
utotoni bali huwa na matokeo hasi kwa watu wazima na kuathiri kipato
chao kwa asilimia 20. Hii inarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Inatarajiwa kuwa asilima 75 ya Watanzania watakuwa wanaishi
katika mazingira safi ifikapo mwaka 2025 na asilimia 100 mwaka 2030.
Mafanikio hayo makumbwa yatafikiwa ikiwa serikali itaendelea kufanya
kazi kwa karibu na washirika wa kimaendeleo wa kimataifa kufanikisha
mpango huo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau wa maendeleo
kutoka Action against Hunger, Aga Khan Foundation-Tanzania, Catholic
Relief Services, Child Investment Fund Foundation, Department for
International Development, Doctors with Africa CUAMM, Embassy of
Switzerland, Feed the Children na Global Affairs Canada.
Wengine
ni Global Alliance for Improved Nutrition, Ifakara Health Institute,
IMA World Health, Institute of International Programs Johns Hopkins
University, and International Fund for Agricultural Development,
International Potato Center, United Nation Children Fund, UN World Food
Program, United States Agency for International Development, World Bank,
World Health Organization na World Vision International.
No comments:
Post a Comment