HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 14 June 2017

USAJILI WA KWANZA KWA YANGA NI HUU, YAANZA NA BEKI WA KATI KUTOKA ZANZIBAR

Meneja wa timu ya Yanga Hafidh Saleh akimkabidhi jezi ya Yanga mchezaji mpya wa timu hiyo Abdallah Haji Shaibu "Ninja" aliyesajiliwa kutoka timu ya Taifa ya Jang"ombe akiingia kandarasi ya miaka miwili.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA wa ligi kuu Vodacom  Tanzania klabu ya Yanga wamefanikiwa kupata saini ya beki wa timu ya Taifa ya Jang"ombe Abdallah Haji Shaibu "Ninja" ambaye walionyesha nia hiyo toka michuano ya Mapinduzi mwezi Januari Visiwani Zanzibar.

Kufanikisha kupata saini ya beki huyo kutoka visiwani Zanzibar, Yanga wanakuwa wamefanya usajili wao wa kwanza toka kumalizika kwa ligi msimu wa 2016/17.

Shaibu amepewa kandarasi ya miaka miwili akitarajiw akurithi mikoa ya Mzanzibar Nadir Haroub ' Canavaro' ambaye ameweza kuitumia klabu ya Yanga kwa takribani miaka 11 toka alivyojiunga.
Beki wa kati Abdallah Haji Shaibu "Ninja"  akiwa anasaini kandarasi ya kuitumika klabu ya Yanga akitokea timu ya Taifa ya Jang'ombe, kushoto ni Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad