HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 June 2017

TSA YAWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAZINGIRA BORA

Mtoto Isam Sepetu (KATIKATI) aliposhika nafasi ya kwanza na kupata medali ya dhahabu akiwa na umri wa miaka 12 katika mashindano ya CANA kanda ya tatu yaliyofanyika Rwanda. Aliwashinda watoto wenzie kutoka Afrika ya Kusini na Zambia.

Na Zainab Myamka, Globu ya Jamii.


CHAMA cha Kuogelea Nchini (TSA) kimewataka wazazi kuwalea watoto katika misingi ya michezo ili kuweza kuwa na afya njema pamoja na mazingira bora.


Hayo yamesemwa leo na Katibu  Mkuu wa Chama cha Kuogelea Nchini (TSA) Ramadhan Namkoveka  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa kila Juni 16  kila mwaka .

Akizungumza na Mtandao huu, Namkoveka amesema kuwa mtoto anatakiwa kulelewa katika mazingira mazuri basi anaweza kuwa na afya njema pamoja na kujijenga kiuwezo katika kufikiria.

"Mtoto akilelewa katika mazimngira mazuri atakuwa na afya njema pamoja na kujijenga kiuwezo katika kufikiria na hilo ndiyo jambo kubwa la msingi," amesema Namkoveka.

Namkoveka amesema kuwa kwa upande wa TSA huwa wanawashauri sana wazazi kuja kuwaleta watoto wakiwa na umri mdogo kwani mchezo wa kuogelea unatakiwa mtoto aanze kujifunza akiwa mdogo kwani wanaanza kuleta ushindani katika mchezo huo.

Amesema, kwa mfano kuna mtoto Isam Sepetu aliweza kupata nafasi ya kwanza na kuondoka na  medali ya dhahabu akiwa na umri wa miaka 12 katika mashindano ya CANA kanda ya tatu yaliyofanyika Rwanda. Aliwashinda watoto wenzie kutoka Afrika ya Kusini na Zambia.

TSA wameshauri wazazi kuweza kuwaacha watoto wao wafanye kila wanachokitaka hususani katika michezo kwani inawapa fursa ya kimichezo na kuepukana na vitendo viovu katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad