HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 June 2017

MKURUGENZI MKUU TMF AFUNGUA MAFUNZO YA KARIKACHA NA VIBONZO JIJINI DAR LEO

Mkurungenzi wa Mkuu wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw. Ernest Sungura aliyekaa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kuchora vibonzo vijana muda mfupi baada ya kuzindua rasmi warsha ya kuwajengea uwezo vijana katika Uchoraji wa Vibonzo, yanayoendelea katika kiota cha wasanii cha NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na asasi ya Nathan Mpangala Foundation (NMF) na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini. Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa NMF, B. Nathan Mpangala wakati kulia kwake ni afisa utawala wa Nafasi Art Space. Mafunzo yatamalizika kesho ambapo Balozi wa Uswis nchini tanzania, bi. Florence Tinguely Mattli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Mwezeshaji Nathan Mpangala, akimwelekeza jambo mmoja wa washiriki wa warsha ya karikacha na uchoraji vibonzo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Penye vibonzo hapakosi tabasamu.
Baadhi ya washiriki wakifanya yao.
Mchoraji, Said Michael maarufu kama ‘Wakudata’ akifanya yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad