HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 16, 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 JIJI LA MBEYA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya alipofanya ziara ofisini hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma 2017.
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima utendaji kazi wa mtumishi.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. Musa Mapunda (wa pili kutoka kushoto) akieleza majukumu ya jiji hilo wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Kaimu Katibu Tawala wa Jiji la Mbeya Bw.Nyasembwa Sivangu akisoma taarifa ya Jiji la Mbeya wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (wa pili kutoka kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba.
Mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiuliza swali wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani) jijini hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) alipofanya ziara jijini hapo mapema leo lengo ikiwa ni kusikiliza changamoto wanazokutana nazo waajiri katika Utumishi wa Umma na kuzipatia ufumbuzi. Ziara hiyo ni moja ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad