HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 15, 2017

KAMPUNI YA KISIWA PURE DRINKING WATER WAGAWA MAJI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

 Meneja mauzo wa kampuni ya Maji safi  ya Kisima, Benito Xavery (katikati) akigawa maji kwa mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kuwa karibu na wadau wao katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, pia ikiwa ni sehemu yakurudisha faida kwa jamii .
   Balozi wa  kampuni ya Maji safi  ya Kisima (kushoto ) akigawa maji safi kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuwa karibu na wadau wao katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, pia ikiwa ni sehemu yakurudisha faida kwa jamii
Mabalozi wa kampuni ya maji safi ya kisima wakiwa tayari kwa kutoa huduma ya kufuturisha  jana maeneo ya fire jijini Dar es Salaam ikiwa ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuwa karibu na wadau wao katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuitambulisha chupa mpya ya maji hayo yenye ujazo wa 0.5L na 1.5L .

Na Mwandishi Wetu.
WATANZANIA Nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia maji yenye viwango hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa madai kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuacha afya zao zikiwa vizuri zaidi kuliko kutia maji yasiyo na viwango kwa madai kuwa kuna baadhi ya maji yanayozalisha lakini yanachunvi nyingi.

Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Aqua Coo ambayo ni Wasambazaji na wazalishaji wa Maji Safi ya Kunywa ya Kisima.

Alisema katika kipindi hiki ambacho waumini wa dini ya kislam wako kwenye mfungo ni vyema wakatumia maji safi na salama ambayo yatawasaidia baada ya mfungo kubaki na afya zao kuliko hali inavyoweza kuwa hapo badaye iwapo watakuwa hawajatumia maji safi.

Meneja huyo, alisema kampuni yake imeamua kuwa na wadau wake wakubwa ambao wanashirikiana nao katika matukio mbalimbali ya kila siku ya ujenzi wa taifa kwa kutoa msaada wa maji ya kunywa hasa nyakati za jioni ili kwa wale wanaokuwa barabarani, kwenye vyombo vya usafiri na mda wa futuru ukafika basi waweze kupata maji hayo wakati wakisubili kufika majumbani mwao.

"Kampuni yetu iligundua kwamba kuna tatizo hasa kwa watu wa imani ya Kiislam ambao kwa wakati huu wanafunga kuwa na tatizo la kupata maji hasa wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri hivyo ikaona ni vyema ijiongeze kwa kutoa maji kwa watu wanaokuwa kwenye magari ili mda ukifika waweze kutumia kinywaji hicho wakati wakisubili kufika majumbani mwao,"alisema Xavery na kuongeza;

"Lakini pia tuliona kwamba kuna umuhimu wa kushirikiana nao kwa ukaribu zaidi na kurudisha kiasi kidogo tunachokipata kwenye jamii yetu ya watanzania,".

Alisema kuwa siyo tu msaada wa maji mwaka huu bali katika Jiji la Dar es Salaam mwaka jana na mwaka juzi waliweza kutoa makoti zaidi ya 3000 kwa mama lishe na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga kutokana na kwamba awali walishindwa kufanya biashara zao kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.

Xavery, alisema pia wanao mpango wa badaye ambapo wanalenga kujitanua zaidi na kwenda Mikoani kwa ajili ya kutoa huduma za kijamii kwa kufanya promosheni kwa matukio mbalimbali ambayo jamii itaona yanafaa ikiwemo misaada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad