Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy inayochakata na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na namna ya kujikinga na majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake kutembelea mradi wa Songas juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika ziara yake juzi.
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna mitambo ya kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.

No comments:
Post a Comment