HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 24, 2017

Tigo yakabidhi msaada kituo cha watoto yatima mkoani Dodoma


Mlezi wa kituo cha watoto cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma Shekhe Mohamed Thabiti (kushoto) akipokea masaada wa vyakula kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) jana kampuni hiyo iliandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

Meneja wa tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) akimkabidhi msaada mtoto Halima Bakari kwa niaba ya watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo ilipoandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5. Meneja wa tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) akishiriki kugawa futari kwa Watoto wa kituo cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo iliandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo wakishiriki futari ya jioni na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo iliandaa futari na kutoa msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi msaada wa chakula na kuandaa futari kwa ajili ya Watoto wanaishi kwenye kituo cha kulelea watoto cha Rahaman Ophanage center cha mjini Dodoma.

Msaada huo ulikabidhiwa jana kwenye kituo hicho na timu ya Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini Aidan Komba .

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo meneja wa Tigo kanda ya kaskazini inayojumisha mikoa ya Dodoma ,Singida na manyara Aidan Komba alisema kampuni ya tigo wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na jamii hasa wenye mazingira magumu.

Komba alisema msaada huo ni sehemu ya faida ambayo kampuni inarudisha kwenye jamii kwa kuwaunga mkono katika kununua na kutumia mtandao wao. Alisema mwaka huu tigo walichagua kushiriki kuandaa futari na kutoa msaada wa vyakula kwa Watoto wanaotunzwa katika kituo hicho ili wao waone kuwa Kampuni inawajali na kushirikiana nao .

Alitaja aina ya vitu walivyokabidhi hapo jana katika kituo hicho kuwa ni mchele ,unga wa ngano,unga wa chakula,mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia na kuogea. Aidha laisema vifaa hivyo walivyokabidhi thamani yake ni zaidi y ash milioni 1.5 na kuwa vyakula hivyo walivyokabidhi vitasaidia kuendelea kupata futari kwa siku za kufunga zilizobaki.

Naye mmoja wa Watoto wanaotunzwa katika kituo cha Rahaman Ophanage Center cha Chang'ombe mjini Dodoma , Halima Bakari aliwashukuru wafanyakazi wa kampuni ya tigo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo mkubwa.

Kwa upande wake mwalimu wa kituo hicho Ustadhi Umas Mafita aliishukuru menejimenti ya kampuni ya Tigo kwa kutoa msaada na kuwapa futari watoto wa kituo hicho

Alitoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa kampuni ya tigo na kijitokokeza kukisaidia kituo hicho chenye watoto zaidi ya 100 wanaotunzwa hapo. Alisema idadi hiyo ya watoto wanaotunzwa pamoja na kupewa mafunzo ya kidini ya kislamu na elimu ya kawaida .

Mafita aliwaomba tigo kuendelea kuwasaidia kituo hicho kwani kinamahitaji mengi kama vifaa vya shule,magodoro, vitanda na ujenzi wa mabweni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad