HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 22, 2017

JUBILEE INSURANCE YAZINDUA SHINDANO LA ISHI HURU, WAKARABATI MIUNDOMINU YA SHULE YA MSINGI MADENGE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Bima ya Jubilee Insurance imezindua kampeni ya ISHI HURU kwa watoto wa darasa la tatu lililoanza Juni 12 na litamalizika rasmi tarehe 30 Juni mwaka huu ikizihusisha shule zote za Serikali.

Katika shindano hili, mwanafunzi wa darasa la tatu atatakiwa kuchora picha zinazoelezea na kuonesha mtazamo wake kuhusu nini maana ya neno ‘ishi huru’ au (live free).

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Bima ya Jubilee, Mhasibu Mkuu Hellena Mzena amesema kuwa Jubilee imeandaa shindano liitwalo ‘Ishi Huru’ au (Live Free), ambalo washiriki watakuwa ni wanafunzi wa darasa la tatu wa shule zote za msingi za serikali.

Hellena amesema washindi wa Tano watakaopatikana watazawadiwa Bima ya Elimu yaani “Jubilee Career Life Cover” watakayoipata watakapojiunga na elimu ya sekondari na kila shule itakayotoa mshindi itapata zawadi ya kikombe (trophies) na cheti cha kutambua ushindi huo.


Akizungumzia kuhusu kampeni ya ukarabati katika shule za msingi mbalimbali, Hellena amesema kampuni ya Bima ya Jubilee imechagua shule za msingi za serikali katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa kutumia vigezo vilivyowekwa na uongozi wake na kugharamia ukarabati wa baadhi ya miundo mbinu ya shule hizo kwa kuzingatia ukubwa wa mahitaji yao. 

Hivyo basi, Shule ya msingi Madenge imekuwa miongoni mwa shule zilizochaguliwa, na hitaji kuu kati ya mahitaji mbalimbali ya miundo mbinu ambalo tulifahamishwa, ni ukarabati wa vyoo na ukuta wa kuzunguka vyoo hivyo. 

Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware, amewapongeza kampuni ya Bima ya Jubilee kwa hatua nzuri waliyoifikia kwa kutimiza miaka 80 toka kuanzishwa kwao na pia kuamua kukarabati miundo mbinu mbalimbali ya shule za msingi.


Saqware amewataka Jubilee kuanza kuwafundisha watoto umuhimu wa kuwa na Bima kuanzia utotoni ili kujijenga na kuelewa maana halisi ya bima kw amanufaa ya baadae.


kampuni ya Bima ya Jubilee imeadhimisha miaka 80 toka kuanzishwa kwake na maadhimisho hayo yanatarjiwa kumaliza mwezi wa nane mwaka huu.
Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Bima ya Jubilee baada ya kuzindua kampeni ya 'Ishi Huru' itakayomalizika Juni 30 mwaka huu pamoja na Mkuu wa Shule ya Madenge Lissy Kaluvya, Diwani na Naibu Meya wa Temeke Feisal ....
Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware pamoha na Mkuu wa Shule ya Madenge Lissy Kaluvya wakizindua shindano la 'Ishi Huru' uliofanyika katika shule hiyo leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugezi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jubilee Life Insurance; Mr. Karim Jamal akizungumza na kuwashukuru Shule ya ,Msingi ya Madenge kwa kuweza kukubali kukarabati shule yao.
Mhasibu Mkuu kampuni ya Bima ya Jubilee Hellena Mzena akisoma risala kwa Mgeni rasmi kuhusiana na kampuni yao ya Jubilee pamoja na jitihjada wanazozifanya katika kuhakikisha wana
Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware pamoja na Mkuu wa Shule ya Madenge Lissy Kaluvya wakimsikiliza moja ya mtoto wa darasa la tatu aliyeingia katika mchuano wa uchoraji wa shindano la Ishi Huru ulizoinduliwa na kampuni ya Bima ya Jubilee.
Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware akikagua maeneo mbalimbali ya shule hiyo yaliyokarabatiwa na Kampuni ya Bima ya Jubilee ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 80 toka kuanzishwa.
Vyoo vilivyokarabatiwa na kampuni ya Bima ya Jubilee vikiwa tayari vimekamilika kukiwa na shimo 12 kwa ajili ya wasichana, vinne kwa ajili ya wavulana na kimoja kwa ajili ya walimu.
Picha na Zainab Nyamka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad