HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 June 2017

DMF, CBA BANK WASHIKIANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU, MBAGALA JIJINI DAR

Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units 106 zilipatikana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wananchi wa Mbagala waliojitokeza katika zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Akizungumza, Mkuu wa Wilaya aliwaasa wananchi kujiwekea utaratibu wa kuchangia damu ili iweze kuhifadhiwa kwenye Benki ya Damu na iweze kuwasaidia wahitaji pale inapohitajika, kwani yeyote anaweza kuwa ni muhitaji wa damu wakati wowote. DC Lyaniva alimalizia kwa kuipongeza taasisi ya Doris Mollel iliyoshirikiana na Benki ya CBA kufanikisha zoezi lililomalizika kwa kupata damu Units 106.
Sehemu ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
Mdau Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.

Mmoja wa wachangia Damu akiingalia damu yake wakati akichangia.
Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.
Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel akijadiliana jambo na mmoja wa waauguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, wakati wa zoezi la uchangiaji Damu, Mbala Rangi Tatu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad