HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 June 2017

AZAM WAMTAMBULISHA ALIYEKUWA MSHAMBULIAJI WA TOTO WAZIRI JUNIOR

Afisa habari wa Azam Jafar Iddy(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha mshambuliaji yao mpya Waziri Junior (wa pili kushoto) aliyesaini kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Toto Afrika Waziri Junior ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari baana ya kusaini kandarasi na timu ya Azam.

Azam jana walifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji huyo kinda kutoka Toto ikiwa ni katika muendelezo wa kuboresha kikosi chao ili kuweza kufanya vizuri katika msimu ujao unaokuja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa habari wa Azam Jafar Iddy amesema kuwa wamefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji juyo kinda kutoka Toto kwani hilo limekuja ikiwa ni moja ya mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo.

"huu ni muendelezo wa kusajili na kufa nya marekebisho katika kikosi chetu kuelekea msimu ujhao, na usajili huu unakuja baada ya kuona mapendekezo ya kocha mkuu Aristoc Cioaba na akwa sasa ni kuwapa fursa vijana,"amesema Iddy

Awali Waziri alikuwa anawaniwa na timu Yanga lakini Azam wameonekana kuwapiga bao na kumsainisha kwa dau nono .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad