HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 2, 2017

AZAM WAACHANA NA NYOTA WENGINE WAWILI, WAMTEMA KAWEMBA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Klabu ya Azam umethibitisha rasmi kuachana rasmi na winga wake Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ame Ally, aliyekuwa kwa mkopo Kagera Sugar ikiwa ni baada ya mapema wiki 
kutoa taarifa ya kuachana na mshambuliaji wao John Raphael Bocco.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa timu ya Azam Jaffar Iddy amesema kuwa wachezaji  wote mikataba yao imemalizika na hawapo katika mipango ya kocha mkuu kwa sasa kwahiyo wameona ni bora watoe taarifa mapema.

Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa klabu hiyo, imeeleza kuwa kuelekea msimu ujao na kuendelea, Azam FC itaweka msisitizo na kufanya uwekezaji ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ ili kuvuna wachezaji bora watakaopandishwa katika kikosi cha timu kubwa.Kwa kuanzia katika kutekeleza malengo hayo, kuelekea msimu ujao Azam FC imewapandisha wachezaji sita kutoka kwenye kituo chake, ambao ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaid, aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Daraja Kwanza (FDL) msimu uliopita kwa mabao 12 aliyofunga alipokuwa kwa mkopo Ashanti United.

Mbali na hilo klabu ya Azam imefanya mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi na katika  hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi ya timu hiyo kwa kukifuta cheo cha Ofisa Mtendaji Mkuu, na sasa cheo cha juu kitakuwa ni Meneja Mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Abdul Mohamed.

Kutokana na mabadiliko hayo ya kiutendaji, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, amemaliza mkataba wake na pande zote mbili zimekubaliana kuachana, na sasa majumuku yake yote yatafanywa na Abdul Mohammed, akiwa ndio Meneja Mkuu wa klabu

Azam FC imekuwa na utaratibu mzuri wa kulea wachezaji wake vijana kwa kuwapandisha kwenye timu kubwa, ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuibeba timu, ambapo wengine waliopo katika kikosi cha wakubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Gadiel Michael, Ismail Gambo, kiungo Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, Himid Mao, Joseph Mahundi na mshambuliaji Shaaban Idd.Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja, anaamini ya kuwa wachezaji hao vijana watazidi kukiimarisha kikosi chake kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu waliopo kikosini, hadi anafikia uamuzi huo wa kuwapandisha aliwafuatilia katika mechi mbalimbali za timu ya vijana ikiwemo na baadhi ya siku kuwajumuisha katika mazoezi ya timu kubwa.Aidha kuhusiana na wachezaji waliomaliza mikataba yao,

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad