HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 17 June 2017

ALIYEPOST PICHA NA VIDEO ZA MAITI AFUNGWA MIEZI MITATU JELA

 Askari Polisi nchini Uingereza, wakimtia mbaroni mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa Jina la Omega Mwaikambo aliyedaiwa kupiga picha ya mwili wa mtu aliyefariki uliokuwemo kwenye mfuko maalum wa kuhifadia maiti inayodhaniwa kuwa ilitokana na ajali ya moto katika jengo la Grenfell Tower iliyotokea hivi karibuni jijini London huko nchini Uingereza kisha kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, alifanya hivyo siku ya jumatano asubuhi, alipotoka nje ya nyumba yake na kukuta mfuko huo wenye mwili na kuufungua kisha kuupiga picha na kurekodi video alizoziweka kwenye mtandao wa Facebook huku akiuliza "Je, kuna mtu yeyote anaujua mwili huu ambao uko nje ya ghorofa langu kwa zaidi ya saa mbili?"

Mtuhumiwa huyo ambaye anaishi eneo la jirani kabisa na jengo la Grenfell Tower lililopatwa na janga la kuteketea kwa moto alipandishwa kizimbani jana Juni 16, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Westminster na kusomewa mashtaka yake na kuhukumiwa kwenda jela kwa miazi mitatu kwa kutenda kosa hilo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad