HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 4 May 2017

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA PALESTINA DR.RIYAD MALIKI,AKARIBISHA KURA YA UNESCO, AKISEMA DUNIA IMEMUA KUSIMAMIA HAKI

Ramallah, Mei 2, 2017 (Wafa) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Dr. Riyad Maliki,Jumanne ya wiki hii amekaribisha matokeo ya kura ya Bodi ya Utendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),kwa kupitisha maazimio mawili yanayohusu Palestina,ambayo ni: Palestina inayokaliwa kimabavu na Taasisi za kiutamadui na kielimu. Nchi zipatazo ishirini (20) zimepitisha maazimio hayo,huku nyingine kumi (10) zikipinga na ishirini na tatu (23) hazikupiga kura.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Maliki amezishukuru nchi hizo zilizopitisha maazimio hayo mawili na kujua wajibu wake katika kuhifadhi maeneo matakatifu nchini Palestina. Alisisitiza kuwa "licha ya jitihada zinazotolewa na serikali kutokana na tamaa ya serikali ya Israeli katika kudhoofisha maazimio ya Palestina ndani ya UNESCO, hata hivyo dunia imepitisha maazimio yetu kwa kuchagua haki iko wapi mbele ya usawa,kazi na sera zake haramu .

Ameongeza kusema kwamba, hilo limethibitisha kushindwa kwa kampeni nyingi za Israeli dhidi ya maazimio yahusuyo Palestina, Jerusalemu na UNESCO, huku wakishindwa pia wale wote waliounga mkono hatua ya kudhoofisha maazimio hayo, miongoni mwa nchi mbalimbali,vikundi,taasisi na hata watu binafsi.

Amesema maazimio yameonesha nyanja za kihistoria, kiutamaduni na urithi wa mji wa Jerusalemu,jambo linalosisitiza umuhimu wa kupeleka mwakilishi wa kudumu wa UNESCO mjini Jerusalemu,ili kufuatilia ukiukwaji na kuondoa vitendo vya uharibifu vinavyofanywa na Israeli,ambayo inafanya juhudi kufuta urithi wa kihistoria,kidini na wa kiutamaduni wa mji huo,hatimae kubadilisha kabisa hadhi yake.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Palestina, kwa upande mwingine ameelezea kutoridhika kwake na msimamo wa nchi zilizokataa kupitisha maazimio hayo mawili,kwa mtazamo wa kushajihisha kuendelea kwa utawala wa kivamizi na vitendo vyake haramu mjini Jerusalemu inayokaliwa kwa mabavu. Pia kushuka kwa misimamo na misingi ya nchi hizi, ambazo baadhi yake zinadai kutetea misingi ya sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Ametilia mkazo kwa kusema, "Sisi tutaendelea kutetea urithi wetu, utamaduni wetu na uwepo wetu,huku tukikabili kampeni zote za kuvuruga hilo na kuziharibu, zinazoongozwa na mamlaka ya kivamizi ya Israeli. Vilevile mapambano ya silaha kwa mujibu wa sheria za kimataifa na matakwa ya taifa la Palestina lenye uwezo wa kujipangia mustakabali wake uliepukana na uvamizi”.

Aidha, ametoa wito kwa mataifa yote duniani kubeba majukumu yao na si kuingilia kazi za UNESCO, wala kuihamasisha Israeli kama ndio taifa la kivamizi kuendelea kufanya maovu yake. Pia Ametoa wito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, hasa UNESCO, kuulinda urithi wa Jerusalemu, utamaduni na historia yake, Jerusalemu ambayo ndio mji mkuu wa Palestina, kutokana hatua zote za kuvuruga ustaarabu wa mji huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad