HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 4, 2017

VIDEO: HUSSEIN MACHOZI AACHIA VIDEO NA WIMBO MPYA ‘NIPE SIKUACHI’

Baada ya kukaa kimya kwa miezi kibao bila kuachia wimbo, Hussein Machozi ameachia wimbo mpya uitwao, Nipe Sikuachi. Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake za Combination Sound.

“Combination yangu ya mimi na Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” anasema Machozi kuhusiana na wimbo huo. “Man Walter ni mshkaji kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona kabisa kwamba sisi tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika,” ameongeza.

Anaeleza, “Video pia imefanyika Italy, Gressoney Italy. Kuna mabadiliko makubwa ukiangalia location ambazo tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona Tanzania za magari na majumba.”

Machozi ambaye anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’, ‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya kimaisha.

“Kama unavyojua, hakuna mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi kadhaa nilishawahi kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya ukosefu wa management.

Kwa sasa Hussein anaishi nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo haimaanishi kuwa ameupa kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya. “Kinachokuja kuonekana sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na nimejaribu kufanya hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu ambacho ni kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba ni kipya, video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”

Video ya wimbo huo ipo Youtube tayari na audio itapatikana mtandaoni

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad