HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 18 May 2017

WAZIRI MHAGAMA KUFUNGUA MKUTANO WA BODI ZA MIFUKO YA HIFADHI

Mh. Jenister Mhagama
NA BALTAZAR MASHAKA.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, anatarajiwa kufungua mkutano wa Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA).

Mkutano huo unaoratibiwa na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) utafanyika jijini Arusha kuanzia Mei 19 na 20, mwaka huu na utahusu ushiriki wa mifuko hiyo kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TSSA Meshack Bandawe alisema mkutano huo utakaofunguliwa na Waziri Mhagama, utashirikisha mifuko saba ya Tanzania bara na mmoja wa Zanzibar.

 Alisema Bodi pamoja na Wakuu wa mifuko hiyo watapata fursa ya  kujadili mafanikio, hatua na maendeleo yaliyofikiwa kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda wenye tija na fursa nchini.

“ Kwenye mkutano huo ambao tumewaalika wadau mbalimbali tutaangalia mafanikio nachngamoto tulizozipata katika uwekezaji wa viwanda kama fursa muhimu hapa nchini,

“Pia tutangalia maendeleo ya ukuaji wa mifuko kiuchumi ili kutuwezesha kutekeleza kwa ufanisi uwekezaji wetu uwe na tija ambao utasaidia kukuza uchumi wan chi,”alisema Bandawe.

Katibu Mkuu huyo wa TSSA alisema kuwa mifuko hiyo imeanza utekelezaji kwwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya viwanda  na baadhi ya miradi hiyo iko kwenye upembuzi yakinifu.
Meshack Bandawe

Alidai kuwa miradi hiyo ikikamilika itatengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania ambao watakuwa wananchama wa mifuko yenyewe  na hivyo kuwa tija katika taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Bandawe  nia ya mkutano huo ni kufikia lengo la uwekezaji wa viwanda na ndiyo maana wamewaalika Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Benki Kuu (BOT),Wizara ya Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango na Msajili wa Hazina.

Bandawe alieleza kuwa TSSA inaundwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni NSSF, PPF,LAPF,GEPF,NHIF,WCF na ZSSF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad