HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 25 May 2017

Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu

 Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(kushoto) akikaribishwa na  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella  alipowasili kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na wadhamni hao na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe akimsikiliza  jambo kwa makini Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(katikati) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana, kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella.
Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi,akiongea wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi mbalimbali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe, akiongea na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali za washindi  wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe,akipewa hongera na Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi baada ya kuongea na wadau walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za washindi  wa Ligi kuu bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017  baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa  tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017  wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi  alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa  ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania  walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alitoa  wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze  wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.

“Kama sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa nchi kwani wanamichezo wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua  yote haya yanawezekana na dalili zimeanza kuonekana.

Alisema  Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo mingine  kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika kutangaza Taifa na pia michezo huchangia  kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.

“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau  timu zote zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa zawadi zao leo.

Ni matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza kuandaliwa  vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,” alisema Hisham.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad