HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 2 May 2017

Upelelezi kesi ya Wema wakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa kuwa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili umekamilika.

Wakili wa Serikali, Onolina Moshi aliyaeleza hayo jana  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mheshimiwa, kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika naomba ahirisho kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH). Amesema Moshi.

Hakimu Simba amehirisha kesi hiyo   hadi Juni Mosi,2017 kwa PH.

Wema amewakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.

Mbali na Wema washtakiwa  wengine ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima. Watuhumiwa hao wawili wanatetewa na wakili Peter Kibatala na Hekima Mwesigwa.

Wema ambaye ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 alifikishwa mahakamani hapo na kupandishwa kizimbani baada ya kusota mahabusu katika kituo kikuu cha Polisi (Police Central ) Dar es Salaam kwa muda wa siku Sita.

Awali ilidaiwa kuwa, Februari 4 mwaka huu, huko Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili.

Hata hivyo washtakiwa hao wote walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad