HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 8, 2017

UFARANSA WAPATA RAIS MPYA, NI KIJANA EMMANUEL MACRON

Emmanul Macron ambaye hakujulikana katika siasa miaka na kabla ya miezi kumi na tatu ya wa uchaguzi wa urais hakua na chama chochote, alichaguliwa Jumapili hii Mei 7 kuwa rais wa nane wa awamu ya tano akiwa na miaka 39.

Emmanuel Macron aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen katika duru ya pili kwa 66.06% ya kura.

 Katika taarifa yake, Emmanuel Macron alisema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa ni raisi mteule. Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa wafaransa waliompa.

Macron pia alitoa shukrani kwa wapiga kura ambao hawakumpigia kura akisema wametekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi waliyemtaka ambapo amesema licha ya yote hayo bado anawaona ni raia wa Ufaransa na wanastahili kusikilizwa.
"Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia , na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa".

Macron alisema jukumu lililoko mbele yake ni kuhakikisha analinda maslahi ya taifa la Ufaransa kwenye umoja wa Ulaya na kwamba kama alivyoahidi wakati wa kampeni anataka kuona Ulaya mpya chini ya uongozi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad