HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 30 May 2017

SHIRIKA LA AFYA NA ELIMU YA TIBA TANZANIA (TAHMEF) LAZIDUA TAWI JIPYA MKOANI MBEYA

Shirika la afya na elimu tiba Tanzania (TAHMEF) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO), lililosajiliwa tarehe 13/09/2015 chini ya mwanzilishi Bi. Juliana Busasi na kuzinduliwa rasmi tarehe 8/7/2016 na Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee Mhe Dr. Hamisi Kigwangalla.

TAHMEF hufanya kazi zake za kuboresha afya na kutoa elimu ya afya kwa kujali maadili na sheria zilizowekwa ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii nzima ya Tanzania. Kwa sasa TAHMEF Imefika zaidi ya watanzania 3,500 katika mikoa mitatu ya Tanzania Bara (Mwanza, Dar es salaam na Pwani) na Mkoa wa Mbeya ndiyo umekuwa mkoa wa nne kufikiwa na shirika hili.
Huduma mbalimbali za afya zinazotolewa ni pamoja na uwiano wa uzito na kimo (BMI),Malaria, shinikizo la damu, sukari, uchunguzi wa awali wa virusi vya ukimwi, saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake, tezi dume kwa wanaume na huendesha kampeni za uchangiaji damu kwa wagonjwa wa selimundu. Pia hutoa ushauri na elimu kwa watu mbalimbali wanaoudhuria kambi, midahalo na matembezi ya hisani juu ya magonjwa mbalimbali jinsi ya kuyaepuka na njia sahihi za matibabu.

Hivi sasa TAHMEF inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio na ajira rasmi na wenye kipato cha chini kuweza kukidhi huduma za afya kupitia bima za afya zitakazotolewa bure kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na kuwapa elimu ya kuwekeza pesa kidogo kidogo ili waweze kujilipia wenyewe kwa miaka inayofuata.
Uzinduzi wa Tawi jipya mkoani Mbeya ni moja kati ya mafanikio ya mipango yao ya TAHMEF ni kumfikia kila mtanzania kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watu juu ya magonjwa mbalimbali jinsi ya kuyaepuka na kuyakabili kuanzia katika shule za elimu ya msingi na sekondari kwa kufanya midahalo mbalimbali.

Uzinduzi huu ulifanyika tarehe 29 mwezi Mei 2017, Katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa kushirikiana na Zahanati ya Senjele na Uongozi wa Kijiji cha Senjele.Uzinduzi huu ulihusisha huduma bure za upimaji wa Afya pamoja na matibabu. Sanjari na hayo uzinduzi huu ulihusisha Elimu ya uhamasishaji wa Kuchangia Damu ambao kilele chake kitaadhimishwa kwa kampeni ya Kuchangia Damu tarehe 10 Juni 2017 mkoani Mbeya.
Shirika hili linatoa Shukrani kwa uongozi wa mkoa huu na kuendelea kuomba ushirikiano ili kufikia watanzania wengi Zaidi kwa huduma hizi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad