HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2017

SERENGETI BOYS KUSHUKA DIMBANI TENA KESHO DHID YA ANGOLA

Na Zainba Nyamka, Globu ya Jamii

Mwamuzi kutoka nchini Ivory Coast Abou Coulibaly anatarajiwa kuchezesha mchezo wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Angola utakaofanyika Uwanja wa l’Amitie kuanzia saa 11.30 jioni kwa saa za Tanzania.

Mwamuzi Coulibaly atasaidiwa na Mamady Tere wa Guinea na Attia Amsaad wa Libya wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Mohamed Maarouf wa Misri huku Kamishna akiwa ni Ismael Locate wa Reunion.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime amesema kwamba ameiona Angola ikicheza na Niger katika mchezo wa kwanza uliofanyika mara baada ya mchezo wa Serengeti na Mali.

“Utakuwa ni mchezo wa ushindani. Nasi tunakwenda kushindana. Matokeo ya awali ya sare kwa timu zote mbili yanafanya mchezo huu kuwa mgumu kwa kundi B.

“Angola ni wa kuchungwa sana. Kwa sababu walipocheza na Niger waliweza kusawazisha mabao mawili kipindi cha pili. Hii inaonesha kuwa ni wepesi wa kusoma makosa yao na kujirekebisha.

“Ila kikosi changu kiko imara, nikiamini kwamba kesho nitapata matokeo mazuri. Watanzania waendelee kutuombea. Tutafanikiwa,” amesema Shime maarufu kwa jina la Mchawi Mweusi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad