HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 27, 2017

Mtoto Anayeongezeka Uzito apelekwa India kwa matibabu

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imemsafirisha mtoto, Antonia Justine Msoka anayeongezeka uzito kwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Mtoto Antonia mwenye umri wa miaka 17 alikuwa amelazwa Muhimbili tangu Novemba mwaka jana na kuanza kupatiwa matibabu.

Akizungumzia afya yake, Antonia amesema kuwa afya yake inaendelea vizuri na amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu.

“Nashukuru kwa msaada kwani sasa naenda Hospitali ya India kwa matibabu zaidi, naishukuru pia serikali kwa kunisadia,” amesema mtoto Antonia.

Awali Antonia alifikishwa Muhimbili akiwa na uzito wa Kilo 250, lakini sasa zimepungua na kufikia kilo 230.

Mama wa mtoto huyo, Salome Manyirizu Kisusi ameishukuru wizara hiyo kwa msaada fedha za matibabu na kumsafirisha kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Nawashukuru watu waliokuwa wakiniombea na pia wote walionichangia fedha za matumizi, Mungu awabariki. Pia, nawashukuru madaktari, wauguzi na uongozi wa Muhimbili kwa ushirikiano mzuri walionipatia,” amesema Mama Salome.
Mtoto Antonia akiwa amepumzika kwenye gari ya kubebea wagonjwa leo kabla ya kupanda ndege kuelekea India.
Baadhi ya wauguzi na madaktari wakimpandisha kwenye ambulance Mtoto Antonia kwa ajili ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad