HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 14 May 2017

MISS USTAWI 2017 KUPATIKANA IJUMAA MEI 19

SHINDANO la Urembo la kumsaka mnyange wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa mwaka 2017/18, linatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa, Mei  19 katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtaa kwa Mtaa jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Warembo hao, Clara Nyaki amesema maandalizi yanaendelea kufanyika kwa ustadi mkubwa huku kila mrembo akiwa ni mwenye hari ya kutaka kunyakua taji hilo, hivyo mshindi atakayepatikana atakuwa ameonyesha uwezo wake binafsi ikilinganishwa na wengine wataofuata.
Clara amesema siku hiyo itakuwa ya kipekee kutokana na namna walivyojipanga  hasa kutokana na urembo walionao warembo wenyewe. Pia, amewakaribisha Watanzania wote kwa ujumla kufika siku hiyo ili kushuduhia tukio hilo.

Kwa upande wao Walimbwende hao wamesema wamejiandaa kila mmoja kuondoka na ushindi kulingana na maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote walichokuwa na mwalimu wao.

Warembo watakaojimwaga siku hiyo ni  Ruth Deouratius ,Melody  Thomas, Elizabeth Julius, Careen Kileo, Loyce Jeck ,Diana Wambura  , Angela  Milanzi pamoja na Elice Mwakajila .
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja kwa pozi mbalimbali watavyokwenda katika kinyanganyilo hicho kitachofanyika Mei 19 katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad